Félix Tshisekedi aliwasili Beijing ju ya kushiriki katika kongamano ya China na Afrika
Rais wa Jamhuri, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, amewasili katika jiji la Beijing, nchini China Jumapili hii ju ya kushiriki katika toleo la tisa la kongamano la ushirikiano kati ya China na Afrika.
Kuanzia Jumatatu hii, Félix Tshisekedi atakuwa na mkutano wa ana kwa ana na mwenzake wa Uchina, Xi Jinping. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya rais, mkutano huu utakuwa wa kwanza kwa Rais wa China kufanya na Mkuu wa Nchi wa Afrika kando ya kongamano hili.
Rais wa Jamhuri ni kiongozi wa ujumbe mkubwa wa Kongo ambao ulisafiri kwenda China. Wajumbe kadhaa wa serikali wako katika kundi yake, akiwemo Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Mawasiliano na Waziri wa Kilimo.
Toleo ya tisa ya kongamano ya ushirikiano kati ya China na Afrika litafanyika kuanzia Septemba tare ine hadi sita, 2024. Mataifa 54 ya Afrika yanashiriki katika mkutano huu na marais na/au wakuu wa serikali 46 watakuwepo Beijing.