Vita Mashariki: Wakuu wa Nchi za EAC wanapiga kura kupinga kuondoka kwa jeshi la kikanda
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado itaunga mkono uwepo wa kikosi cha kanda ya EAC katika sehemu yake ya mashariki. Ombi la serikali ya Kongo limekataliwa hivi punde na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Ijumaa hii, Novemba makumi mbili na ine nchini Tanzania.
Hakuna ata kalendari ya kuondoka kwa jeshi la kikanda imewasilishwa. Wakuu wa Nchi walipendekeza mashauriano kati ya wakuu wa majeshi wa EAC na SADC.
Mapendekezo haya, kulingana na mahitimisho ya mkutano wa makumi mbili na tatu, lazima yawasilishwe kwa mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama kabla ya mkutano ujao wa shirika la kikanda.
Mkutano huo pia umezitaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jamhuri ya Rwanda, Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuharakisha kukamilika kwa mashauriano ya kitaifa kuhusu Shirikisho la Kisiasa la EAC ifikapo tarehe makumi tatu Mei, 2024.
Akitangazwa nchini Tanzania kwa dakika ya makumi mbili na tatu, Mkuu wa Nchi aliwakilishwa na Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi wa Taifa, Jean-Pierre Bemba Gombo.