DRC: Judith Suminwa Tuluka ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Yeye ndiye kiongozi mpya wa serikali ijayo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Judith Suminwa Tuluka, aliyeteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Tshisekedi chini ya agizo lililosomwa Jumatatu hii, Aprili taré moja 2024.

Redaction

2 mwezi ya iné 2024 - 13:48
 0
DRC: Judith Suminwa Tuluka ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Yeye ni nani?

Asili kutoka Kongo ya kati, Judith Suminwa alizaliwa Oktoba taré kumi na kenda, 1967.

Ana shahada ya uzamili katika uchumi uliotumika kutoka Chuo Kikuu Huria cha Brussels na diploma ya masomo ya ziada katika kazi katika nchi zinazoendelea.

Alifanya kazi kwa muda mrefu katika sekta ya benki kabla ya kujiunga na mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo PNUD ambayo alikuwa mtaalamu wa kitaifa katika mradi wa kusaidia jamii mashariki mwa nchi. Kisha alifanya kazi katika afisi ya Wizara ya Bajeti kabla ya kuwa naibu mratibu wa baraza la ufuatiliaji wa mikakati ya rais.

Machi taré makumi mbili na ine, 2023, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Waziri wa Mipango katika serikali ya Sama Lukonde II.

Mnamo Aprili taré moja, aliteuliwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu na Rais wa Jamhuri, Félix Tshisekedi na kuchukua nafasi ya Jean-Michel Sama Lukonde, aliyeteuliwa Aprili 26, 2021.

Judith Suminwa Tuluka hivyo anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Waziri Mkuu.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.