DRC: serikali inazindua kampeni ya « wote kwa Nchi ya Baba » ju ya kupambana na uvamizi wa Rwanda
Serikali ya Kongo ndiyo imezindua kampeni ya « wote kwa Nchi ya Baba »kukabiliana na uvamizi wa Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mawasiliano wakati wa mkutano huo uliofanyika katika mji wa Kisangani Ijumaa hii, taré mbili Agosti .
Kulingana na Patrick Muyaya, kampeni hii inalenga kutumia rasilimali « tulizo nazo kupigana kwa pamoja na kibinafsi uchokozi huu na wale wote wanaojifanya kuwa maadui wa maendeleo ya nchi yetu. »
« Kwa kuzindua kampeni hii ya kutetea nchi, tunataka kuwaambia kila Mkongomani popote alipo ni kiasi gani kujitolea kwao ni muhimu katika pambano hili la pamoja »alisema.
Waziri wa Mawasiliano hakuwa peke yake mbele ya waandishi wa habari. Mgeni wa mkutano huo, msemaji wa jeshi Jenerali Sylvain Ekenge alituma ujumbe wa faraja kwa wanajeshi wa Kongo wanaolinda mipaka ya jamuhuri ya kidemocratia ya kongo.
« Nguvu za adui zinaweza kuonekana haziwezi kushindwa, lakini nakuambia sisi ni zaidi ya askari. Sisi ni washairi wa upinzani (…) adui anaweza kuwa na mizinga, ndege, lakini hana roho zetu. Risasi zetu ni maneno. Vilio vyetu ni mashairi. Kila risasi ni aya katika hadithi ya epic ya uhuru wetu. Nguvu ya ndoto ni halisi, lakini haiwezi kuzima moto wa maisha unaowaka ndani yetu. Angalia pande zote, »alisema.
Kampeni hii mpya iliyozinduliwa na serikali inakuja baada ya "Bendele ekweya te" kufuatia uvamizi wa Wanyarwanda katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
