DRC: Patrick Muyaya atazindua wiki ya film ya China
Studio ya Mama Ngebi ya RTNC ilitumika kama eneo ya uzinduzi wa wiki ya film ya Kichina na Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari na msemaji wa serikali, Patrick Muyaya, Jumatatu Agosti tare tano apa Kinshasa.
Katika maneno yake, Patrick Muyaya alirejea mtindo wa China uliotolewa na balozi wa China nchini DRC b
Ju ya kusifu utamaduni wa Kongo unaozingatia mila na desturi za mababu zake.
"Unaweza kuwa na uhakika kwamba tumejitolea kuhifadhi maadili na mila zetu za Kongo, na kujenga nchi nzuri zaidi ambapo uwezo wa utalii pia ni mkubwa," alisema.
Kwa Balozi wa China nchini DRC, Zhao Bin, tukio iyi inaimarisha mahusiano ya pande mbili zilizopo kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo yana pointi kadhaa sawa katika historia yao. Kupitia televisheni ya umma nchini DRC, inabainisha ujumbe kutoka kwa Wizara ya Mawasiliano, inakuza utamaduni wa Kichina, hasa maadili ya kawaida yanayoshirikiwa kati ya Kinshasa na Pékin.
Watu kadhaa walishiriki katika shughuli hii, akiwemo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Urithi Yolande Elebe; Waziri wa Utalii Didier M'pambia; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Eugénie Tshiela pamoja na kamati ya usimamizi ya RTNC. Wiki ya film ya China iko chini ya mada: "Urafiki wa Sino-Kongo: maadili ya kawaida, siku zijazo ya pamoja".
