DRC : serikali inajitahidi kunusuru kikapu kya wa mama nyumbani
Kuimarisha uwezo wa ununuzi wa idadi ya watu wa Kongo ilikuwa katikati ya mawasiliano ya serikali kwa waandishi wa habari, Siku ya kwanza Agosti taré kumi Na mbili, 2024 wakati wa mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari.
Kwa Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Uchumi wa Kitaifa, wakati umefika kwa serikali ya Kongo "kupunguza kikapu kya wa mama Wakongo", kwa kuimarisha uwezo wa ununuzi wa idadi ya watu.
“Tunafahamu kuwa maamuzi haya yataigharimu Serikali ki fedha. Chaguo lilifanywa kati ya gharama hii na kupunguza kikapu cha mama wa nyumbani. Wakati umefika wa kupunguza kikapu cha mama wa nyumbani. Hii, kwa njia sawa na ambayo uchaguzi umefanywa, kwa miaka kadhaa, kati ya kuwafanya Wakongo walipe bei halisi ya bidhaa ya petroli na mapato ya serikali. ", alisema.
Profesa Mukoko Samba Daniel alitumia fursa ya ziara yake kukumbuka mchango mkubwa wa serikali kuu katika ununuzi wa kila lita ya mafuta inayonunuliwa kwenye pampu .
"Ikiwa serkali halingetoa kiasi cha 2,300 CDF kwa lita moja ya mafuta iliyonunuliwa na watumiaji kwenye pampu, bidhaa zote zingegharimu zaidi, kuanzia na huduma ya usafirishaji.
Mawasiliano haya kutoka kwa serikali yanafuata maagizo ya Rais wa Jamhuri yanayolenga kuondoa ushuru kwa baadhi ya bidhaa muhimu zinazoagizwa kutoka nje, yaliyowasilishwa wakati wa mkutano wa mwisho wa wiki wa Baraza ya Mawaziri.
Uamuzi huu kimsingi unalenga kupambana na gharama ya juu ya maisha ya kila siku katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kushuka kwa thamani ya faranga ya Kongo ju ya sarafu ya Marekani kunaathiri pakubwa bei za bidhaa sokoni.
