Mpox: DRC inavuka kizingiti cha vifo miya sita (600)
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongokwa sasa inaesabu vifo miya sita na kumi (610) kufuatia janga ya Monkeypox ambalo inaathiri majimbo kadhaa. Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Roger Kamba.
Roger Kamba pia aliripoti kuwa tangu Januari, kesi 17,801 zinazoshukiwa zimeripotiwa katika mikoa iliyoathiriwa, na kiwango cha vifo vya kesi 3.5%.
Mikoa iliyoathiriwa zaidi katika Magharibi ni Equateur, Ubangi Kusini, na Maï-Ndombe, wakati Mashariki, ni Kivu Kusini na Kaskazini. Maeneo yanayokaliwa na magaidi pia yameathirika lakini hayawezi kuungwa mkono kutokana na ukosefu wa usalama.
