DRC: Félix Tshisekedi atoa wito kwa watu wanaoishi nje ya Kongo kurejea nchini
Rais wa Jamhuri, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, alizungumza na diaspora wa Kongo wanaoishi Ufaransa Jumatatu hii, Julai taré makumi mbili n'a kenda, 2024 mwisho mwa kukaa kwake katika nchi hii.
Kwa maneno yake, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alirudilia wito wake kwa wana diaspora wa Kongo warejea kuishi nchini humo ili kuchangia maendeleo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
« Jipangiye kurejea nyumbani kushiriki katika maendeleo ya nchi yako » Félix Tshisekedi alisema akisindikizwa na shangwe kutoka kwa umma.
Mada kadhaa zilijadiliwa katika mijadala hii. Kuhusu GO PASS katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa N’Djili, Felix Tshisekedi anapendelea kwamba ushuru huu utumike “kwa busara na si kama zamani katika mifuko ya maadui wa Kongo”.
Kulingana na Top Congo, Rais Tshisekedi, hata hivyo, aliahidi kuchunguza suala hilo, akibainisha kuwa « hatari ni kwamba GO PASS inapatikana katika bei ya tiketi »
