Vita Mashariki: Kikosi kipya cha wanajeshi miya nane(800) tsha Burundi walitumwa Kivu Kusini

Kikosi kipya cha wanajeshi miya nane tsha Burundi kimetumwa katika mkoa wa Kivu Kusini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilitangaza vyombo vya habari vya ndani na RFI (Radio France Internationale).

Redaction

18 mwezi wa kenda 2023 - 12:35
 0
Vita Mashariki: Kikosi kipya cha wanajeshi miya nane(800) tsha Burundi walitumwa Kivu Kusini

Kikosi hiki kipya kimeongezwa kwa vile vingine vitatu vilivyopo tayari na vikosi vingine viwili ambavyo tayari vimewekwa kwenye kambi ya kijeshi ya Mudubugu.

Kutumwa kwa jeshi la Burundi nchini DRC ni matokeo ya mkataba mpya uliotiwa saini kati ya Tshisekedi na Ndayishimiye mwishoni mwa mwezi Agosti mjini Kinshasa.

Nchi hii leo, kama sehemu ya kikosi cha EAC, ina vikosi vinne au karibu wanajeshi elfu tatu miya mbili (3,200) katika sehemu hii ya DRC na kikosi kingine kilichotumwa Kivu Kaskazini kwa ombi la Kinshasa, RFI ilionyesha.

Burundi inasalia, hadi itakapothibitishwa vinginevyo, mshirika mwaminifu pamoja na DRC, inakabiliwa na uchokozi wa jeshi la Rwanda na waasi wa M23, ambao wanadhibiti sehemu ya eneo la kitaifa la Kongo katika sehemu yake ya mashariki.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.