DRC: Kuanzia Jumatatu hii apa Kinshasa kwenye meza ya duara ya hali ya kuzingirwa huko Kivu Kaskazini na Ituri.

Kinshasa itapokeya kuanzia Agosti taré kumi na ine hadi kumi n'a sita , meza ya duara ya tathmini ya hali ya kuzingirwa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri, kwa uamuzi wa Rais wa Jamhuri, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo.

Redaction

14 mwezi ya nane 2023 - 09:25
14 mwezi ya nane 2023 - 09:26
 0
DRC: Kuanzia Jumatatu hii apa Kinshasa kwenye meza ya duara ya hali ya kuzingirwa huko Kivu Kaskazini na Ituri.

Mukutano hii italeta pamoja, katika Ikulu ya Watu, vyama kadhaa ikiwa ni pamoja na wataalam kutoka kwenye Urais, wajumbe wa serikali, watendaji wa kisiasa na kiraia na huduma za usalama.

Watu kadhaa wanachagua kuondolewa kwa hali ya kuzingirwa katika majimbo hayo mawili. Hii ni kesi ya gavana wa zamani wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku, Waziri wa sasa wa Viwanda.

"Hakuna kitu kingine kinachotarajiwa kutoka kwa mkutano uyu isipokuwa tu kuondolewa kwa hali ya kuzingirwa. Tulifanya tathmini tatu na mahitaji makubwa yalikuwa ni hali ya kuzingirwa kuondolewa,” alisema.

Majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri yamekuwa yakizingirwa kwa miaka miwili. Watu kadhaa waliuawa katika kipindi hiki ijapokuwa kuliwekwa mipango ya kijeshi kuimarishwa.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.