Uchaguzi wa urais wa 2023:  Seth Kikuni anaomba Mahakama ya Kikatiba kubatilisha ugombea wa Tshisekedi kwa "ukosefu wa ubora na uwandishi  wa huwongo"

Mawakili wa mpinzani Seth Kikuni wameikamata Mahakama ya Kikatiba Jumatatu hii, Oktoba makumi mbili na tatu kuomba kubatilisha ugombea wa Félix-Antoine Tshisekedi, kwa kukosa ubora na uwandishi wa huwongo.

Redaction

24 Mwezi wa kumi 2023 - 09:22
 0
Uchaguzi wa urais wa 2023:  Seth Kikuni anaomba Mahakama ya Kikatiba kubatilisha ugombea wa Tshisekedi kwa "ukosefu wa ubora na uwandishi  wa huwongo"

Kulingana na ombi la Kikuni, Tshisekedi alitangazwa mwaka wa 2019 na utambulisho wa "Tshisekedi Tshilombo Félix" huku kwenye orodha iliyochapishwa na CENI mwaka huu, jina lake ni "Tshisekedi Tshilombo Félix Antoine".

Mawakili wa Seth Kikuni wanaikumbusha Mahakama kwamba jina, jina la baada ya jina na jina la kwanza la kila Mkongo "havibadiliki", kama ilivyoainishwa na kanuni ya familia katika kifungu cha makumi Tano n'a sita 

Baraza la rais wa chama cha siasa PISTE pia lilitoa fursa kwa mahakama vipengele vinavyounda sheria ya kesi katika suala hili, kubainisha kesi chache zinazofanana na hizo ambazo zilisababisha kubatilisha ugombea fulani.

Moise Katumbi sasa si mgombea pekee aliyeshambuliwa katika Mahakama ya Kikatiba. Mahakama ya juu zaidi ya Kongo inatarajiwa kutoa uamuzi katika siku zijazo.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.