DRC: Félix Tshisekedi anahadi kukarabati kilomita 38,000 za ma barabara ya huduma ya kilimo mnamo 2025
Rais wa Jamhuri, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo, anajitolea kukarabati, kwa jumla, kilomita elfu thelathini na nane (38,000) ya huduma ya kilimo katika eneo lote mwaka wa 2025, kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo.
Rais Tshisekedi pia anajitolea kukarabati kilomita 11,423 ya kipaumbele katika mwaka mmoja. Mkuu wa Nchi, ju ya kutimiza ahadi hii, atapeleka brigedi katika kila mkoa ili kutekeleza kazi hiyo.
"DRC ni eneo kubwa la ujenzi, nchi inayoendelea ambayo inajenga mustakabali mzuri, na huu ni mwanzo tu," alisema, akimaanisha uwekezaji wenye thamani ya dola milioni kadhaa za Marekani, na hivyo kutengeneza ajira kadhaa.
Félix Tshisekedi pia anakusudia kufanya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Ndani unaozingatia maeneo miya makumi ine na tano (PDL145 T) kuwa kipaumbele kikuu katika mwaka wa 2025.
