DRC: barua  mpya ya waendesha gari itapatikana mwishoni mwa 2024 [Jean-Pierre Bemba]

Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Jean-Pierre Bemba alikuwa na kikao cha kazi na Bob Amiso, Waziri wa Uchukuzi wa Mkoa wa Kinshasa, Agosti makumi mbili na nane katika mji mkuu wa Kongo. 

Redaction

29 mwezi ya nane 2024 - 20:13
29 mwezi ya nane 2024 - 20:14
 0
DRC: barua  mpya ya waendesha gari itapatikana mwishoni mwa 2024 [Jean-Pierre Bemba]

Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo, Jean-Pierre Bemba alimtangazia mwenyeji wake kuwa serikali kuu inaweka juhudi yote katika kuwapatia wananchi barua mpya ya udereva. 

Kwa upande wake, Waziri wa jimbo Bob Amiso alimweleza VPM Jean-Pierre Bemba azma yake ya kuweka huduma ya usafiri ya jiji ya Kinshasa kwenye kidijitali, ili kuhakikisha usalama barabarani na kutatua matatizo kadhaa katika sekta hii. 

Ukarabati wa reli

Msongamano kubwa ambayo imeikumba Kinshasa hivi majuzi haijawatoroka mawaziri hao wawili. Jean-Pierre Bemba na Bob Amiso walikubali kukarabati reli hiyo iliyoko  Avenue belgika

Ju ya kufanya hivyo, Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Uchukuzi na Waziri wa Uchukuzi wa Mkoa waliamua kufanya kazi kwa pamoja ju kufanikisha mradi huu ambao unalenga kuunganisha katikati ya jiji na magharibi mwa Kinshasa.

Mradi huu unafuata nyayo za Kin Metro, mradi ambao pia unalenga kuboresha trafiki katika jiji ili kuepuka msongamano wa magari katika mji mkuu.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.