Mjadala kuhusu marekebisho ya Katiba: « Ninachokiona ni shambulio kwa Rais wa Jamhuri » Muyaya kwa upinzani
Nyuma ya msimamo uliotolewa na baadhi ya wadau wa siasa ambao ni wanachama wa upinzani, akiwemo Delly Sesanga, kuhusu marekebisho ya Katiba, Patrick Muyaya anaona mashambulizi ya ghafla ju ya Rais wa Jamhuri “kwa kutumia Katiba kama kisingizio”.
Akikabiliana na waandishi wa habari Siku ya kwanza tare kumi na nane Novemba mjini Lubumbashi, msemaji wa serikali Patrick Muyaya alisema ameshangazwa na majibu hayo, hasa kutoka kwa Delly Sesanga, wakati wahusika kadhaa wa kisiasa hapo awali, waliunga mkono mradi wa kurekebisha baadhi ya vifungu vya Katiba.
“Hapa, ni lazima tutoke kwenye chuki, uchungu, upande wa kijicho au upande wenye tamaa ya kupita kiasi ya kuwa Rais wa Jamhuri kwa gharama yoyote ile Ninachokiona ni kutochoka kwa Rais wa Jamhuri kwa kutumia Katiba kama kisingizio,” alisema.
Pia alialika vyama mbalimbali kukuza uwiano wa kitaifa badala ya chuki, huku akisubiri kuanzishwa, mwaka 2025, kwa tume yenye jukumu ya kukusanya maoni ya Wakongomani kuhusu marekebisho ya Katiba, "yanayoeleweka kwa wale wanaosema hapana."
Mijadala ya marekebisho ya Katiba inazidi kuwa mikali. Ikiwa UDPS iko katika oveni na kinu kwa ajili ya marekebisho ya Katiba, vyama vingine wanachama wa urais wa Muungano Mtakatifu ikiwa ni pamoja na UNC na MLC hudumu kimya.
