DRC: Adolphe Muzito anafunga kampeni yake ya mawasiliano apa mjini Kinshasa

Mgombea urais wa Jamhuri, Adolphe Muzito, amefunga kampeni yake ya ndani Alhamisi hii, Novemba makumi tatu, katika mji wa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Redaction

30 Mwezi wa kumi n'a moja 2023 - 19:58
 0
DRC: Adolphe Muzito anafunga kampeni yake ya mawasiliano apa mjini Kinshasa

Kwa siku hii ya mwisho, Adolphe Muzito na wasaidizi wake walianza kampeni hii ya mtaa katika wilaya ya Kimbanseke. Katika kile kinachojulikana kama soko la miaka hamsini, Waziri Mkuu wa zamani alipokea malalamiko kutoka kwa wauzaji kuhusu masharti yao ya kuuza.

Mgombea nambari makumi mbili na ine( 24) katika uchaguzi wa urais mnamo Desemba makumi mbili  aliendelea na ziara yake katika mji jirani wa Masina ambapo umati wa watu ulimkaribisha. Katika wilaya ya Mapela, Adolphe Muzito alihisi hali ya reli na hali ya maisha ya watu hawa.

Baada ya wilaya ya Tshangu, naibu huyo wa zamani wa kitaifa alifunga kampeni yake ya ndani katika wilaya ya Mont-Amba. Katika wilaya ya Kisenso, kila mahali alipoenda, mgombea nambari 24 alihubiri programu yake juu ya upanuzi wa jiji la Kinshasa katika sehemu yake ya mashariki.

Mpango huu unalenga kujenga miundombinu ya makazi ya kijamii, afya na utawala katika manispaa za Nsele na Maluku kwa lengo la kutengeneza nafasi zaidi ya milioni kumi na mbili (12 )za ajira kwa wakazi wa Kinshasa.

Adolphe Muzito alianza kampeni yake ya kuwafikia watu Jumatano, Novemba 29 katika wilaya za Funa na Lukunga. Katika upande  uyu wa mji mkuu, Waziri Mkuu wa zamani alihubiri mradi wake unaolenga kuboresha hali ya maisha ya watu.

Redaction UNE.CD est un média en ligne basé à Kinshasa, capitale de la République Démocratique du Congo, qui collecte, traite et diffuse des informations générales de la RDC, l'Afrique et le Monde. Grâce à nous, l'actualité vous suit partout en temps réel sur votre téléphone, tablette et ordinateur en un seul clic.